Beninyo wa Dijon (kwa Kilatini: Benignus; kwa Kifaransa: Bénigne, Benin na Broingt; Smirna, leo nchini Uturuki, karne ya 2 - Dijon, leo nchini Ufaransa, 179) alikuwa padri ambaye aliinjilisha mkoa wa Burgundy na hatimaye alifia dini ya Ukristo huko[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Novemba[2][3].